The sports Hub

Ajib awaza ubingwa Yanga

0 22

LICHA ya Wanayanga wengi kuanza kuwa na wasiwasi nae nahodha wa klabu hiyo, Ibrahim Ajib mwenye ufundi mwingi wa kuchezea mpira na kutengeneza mabao amesema amesikia maneno ya chini chini kwamba ana mpango wa kujiunga na Simba.

Nyota huyo ambaye alikosa mechi kadhaa za ligi kuu kutokana na kusumbuliwa na nyama za paja alisema bado ana mkataba na Yanga na mawazo yake kwa sasa ni kuisaidia klabu yake hiyo kutwaa ubingwa msimu huu.

“Bado nina mkataba na Yanga kwa sasa hivyo hizo taarifa nyingine zinazoenea huko mitaani mimi sizijui kabisa, kilichopo kichwani mwangu kwa sasa ni kuipigania timu yangu kutwaa ubingwa msimu huu na kuwafanya mashabiki wetu wafurahi,” alisema.

Maneno hayo ya Ajib bila shaka yanajibu kiu ya mashabiki wake,

ambao wamekuwa roho juu baada ya kuenea taarifa kwamba Simba wanafanya mipango ya chini kwa chini ya kumchukua.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.