Kitaifa

Alichotamka Dismas Ten baada ya kukabidhi ofisi Mbeya City

on

Dismas Ten kushoto akiwa na Mussa Mapunda baada ya makabidhiano ya ofisi

 

ALIYEKUWA afsa habari wa Mbeya City FC, Dismas Ten amekabidhi rasmi ofisi kwa mwenyekiti wa wagonga nyundo hao, Mussa Mapunda katika kikao maalum kilichofanyika kwenye ofisi za halmashauri ya jiji la Mbeya mchana wa leo.

Makabidhiano hayo yamekuja baada ya afsa habari huyo anayesifika kwa ubunifu kibiashara kuingia mkataba na mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom anakoenda kuwa mkuu wa idara ya habari na mahusiano akisaidiwa na Godlisten Anderson ‘Chicharito’.

Akizungumza na BOIPLUS mara baada ya makabidhiano hayo Ten anayetarajiwa kuanza kazi rasmi Ijumaa Julai 21 alisema baada ya kumalizana na Yanga alirejea Mbeya kwa ajili kukabidhi ofisi na kuagana na viongozi na wadau wa timu hiyo aliyoitumikia kwa uadilifu mkubwa katika kipindi cha miaka minne.

“Nipo Mbeya kwa ajili ya kufanya makabidhiano ya ofisi, kipekee naushukuru sana uongozi wa MCC, mashabiki na wadau wote kwa namna ambavyo tumeshirikiana kuifanya timu hii kuwa na sura ya kimataifa.” Alisema Ten.

Akizungumzia changamoto anazoweza kukutana nazo kwa kubadili mazingira ya kazi Ten alikiri hizo haziwezi kukosekana kwa sababu Yanga ni timu kubwa kuliko City lakini akisisitiza kila kitu kitakwenda sawa.

Dismas Ten (kulia) akiwa na msaidizi wake Godlisten Anderson ‘Chicharito’ siku waliyotambulishwa mbele ya waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga

“Changamoto hazikwepeki hapo kwavile Yanga ni kubwa kuliko MCC lakini tayari kwa kushirikiana na uongozi wa Yanga tumeweka
lengo la kuleta mfumo mpya au mapinduzi kwenye eneo la upashanaji habari za klabu kwa kuzingatia weledi.

“Lakini pia tumejipanga kuhakikisha idara inakuwa sehemu ya mlango wa klabu kuingiza mapato, kwahiyo wanayanga watuunge mkono katika kuhakikisha malengo yaliyowekwa yanafikiwa,” alimaliza Ten.

Kwa upande wake mwenyekiti wa City, Mapunda alisema;

“Tunamtakia kila la kheri kwenye majukumu yake mapya, tumekuwa pamoja kwa miaka minne tunashukuru kwa mchango wake, hakika amefanya kazi kubwa, hili liko wazi na kila mmoja anatambua, hapa ni nyumbani asisite kukaribia wakati wowote, sisi tuko tayari kumpokea.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *