Kitaifa

Alichotamka Kotei baada ya kusaini mkataba mpya Simba

on

BAADA ya kiungo Mghana wa Simba, James Kotei kusaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia klabu hiyo, ametoa kauli ambayo wanasimba wengi walikuwa wakiisubiri kwa hamu.

Akizungumza na BOIPLUS Kotei ameelezea furaha yake kubakia Msimbazi huku akitamka kuwa ni wakati wake wa kupiga kazi ndani ya kikosi hicho.

“Nimefurahi sana kusaini mkataba mpya, hii ni timu ambayo mashabiki wake wana upendo sana. Naamini viongozi wameona mchango wangu ndio sababu wamenipa mkataba, sasa huu ni wakati wa kuchapa kazi.

“Nimesaini mkataba wa miaka miwili, kutokana na furaha niliyonayo naahidi kuongeza juhudi ili kuhakikisha nafanya vizuri zaidi ya mwanzo,” alisema Kotei.

Kotei alimaliza mkataba wake wa miezi sita na Simba ambapo walishindwa kumpa mkataba mrefu kwa madai ya kutaka kujiridhisha kwanza na kiwango chake jambo ambalo amelithibitisha kwa vitendo baada ya kuwa msaada mkubwa kwa kipindi chote alichokuwepo ndani ya Simba.

Simba hawakuwa na haraka ya kumwongeza mkataba mpya mchezaji huyo hata baada ya kuwepo na taarifa za watani wao kuhitaji huduma ya Kotei.

Hivi karibuni Yanga walikuwa wanasaka saini ya mchezaji huyo lakini walishindwa kuipata kutokana na Kotei kuwa na msimamo wa kuipa nafasi ya kwanza Simba ambayo ni timu ya kwanza kumleta nchini.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *