Kitaifa

Alichotamka Ndumbaro baada ya kuachiwa huru

on

WAKILI Damas Ndumbaro amerejea kwa kishindo katika medani ya soka baada ya kuachiwa huru na kamati ya rufaa ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) asubuhi ya leo.

Ndumbaro alifungiwa kutojihusisha na masuala ya soka kwa miaka saba kufuatia kushindwa kufuata maagizo ya TFF wakati akiwa Wakili wa klabu zinazoshiriki ligi kuu Tanzania bara.

Ndumbaro ameiambia BOIPLUS kuwa ameshukuru Kamati hiyo kutenda haki kwa kumuacha huru huku akiwa ameshatumikia adhabu hiyo kwa miaka miwili na miezi tisa.

“Nimerejea rasmi katika mpira, kikubwa naishukuru kamati kwa kutenda haki. Sina chuki na mtu yeyote kilichotokea ni sehemu ya maisha,” alisema Ndumbaro.

Mwenyekiti wa kamati ya rufaa ya TFF, Rahim Shaban

Mapema asubuhi ya leo Mwenyekiti wa kamati ya rufaa ya TFF, Rahim Shaban aliwaaambia Waandishi kuwa Ndumbaro aliomba mrejeo wa hukumu yake (Review) baada ya kuona hakutendewa haki kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri na aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu kwa wakati huo Wakili Jerome Msemwa.

“Ndumbaro aliomba review baada ya kutoelewana Msemwa ambaye alikuwa Mwenyekiti na kamati iliyomuhukumu kwahiyo kamati imejiridhisha na kumuachia huru baada ya kupitia vizuri hukumu hiyo,” alisema Rahim.

Nae aliyekuwa kocha msaidizi wa timu ya Geita gold Mining, Choki Abeid ameachiwa huru baada ya kuhukumiwa kifungo cha kutojihusisha na soka maisha huku Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Tabora, Yusuph Kitumbo akiendelea kutumikia adhabu yake ya kufungiwa maisha.

Wengine watakaoendelea na adhabu za kufungiwa maisha ni viongozi wa timu ya JKT Oljoro ya Arusha Frechi Rwentula na Thomas Mwita kutokana na kashfa za upangaji wa matokeo kwenye soka.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *