Kitaifa

ALLY SHOMARI: Nimekuja Simba Kucheza Sio Kukaa Benchi

on

NYOTA mpya wa timu ya Simba Ally Shomari amesema hatishwi na aina ya wachezaji wanaosajiliwa na Wekundu hao huku akijipanga kumshawishi kocha kwa kujituma uwanjani ili kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Shomari ambaye anaweza kucheza nafasi nyingi uwanjani (kiraka) kama beki, winga au kiungo amejiunga na Simba akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro ambako alikuwa ni mchezaji wa kutegemewa lakini kwa Simba inaweza ikawa tofauti kutokana na ushindani wa namba uliopo.

Shomari ameiambia BOIPLUS kuwa amejiunga na Simba kwa ajili ya kwenda kucheza mpira na sio kutazama wenzake japokuwa amekiri atakutana na upinzani wa namba lakini jambo hilo halimnyimi usingizi.

“Simba ina wachezaji wazuri na inaendelea kusajili wengine, hilo kwangu haliniumizi kichwa ninachojua ni kufanya mazoezi, kujituma na heshima ndio kitu ambacho ninaamini kitamfanya kocha kunipa nafasi,” alisema Shomari.

Kiraka huyo alisema nia yake ni kucheza timu ya Taifa na kujiunga na Simba kutamfanya aonekane zaidi ambapo ataweza kutoa mchango wake kuisaidia kufanya vizuri.

“Ni dhamira ya kila mchezaji kuchezea timu ya Taifa kwangu pia ni hivyo hivyo, naamini kupitia Simba nitaweza kufanikiwa kupata nafasi ya kulitumikia taifa langu”.

Tayari Simba imemsajili beki wa kulia Shomari Kapombe kutoka Azam FC ambapo kutakuwa na upinzani mkubwa wa namba katika nafasi hiyo kutokana na uwezo mkubwa walionao wote wawili.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *