Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

Alphonce Modest Aendelea na Matibabu Muhimbili

0 340

MCHEZAJI wa zamani wa kimataifa aliyezichezea Simba SC, Pamba, Yanga SC pamoja na Mtibwa Sugar Alphonce Modesti alifikishwa kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili jana kwa matibabu akiwasili kutoka Morogoro kwa gari ya wagonjwa inayomilikiwa na kiwanda cha sukari cha Mtibwa.

Modest anasumbuliwa na maradhi ya kupooza kwa takribani miaka mitano sasa. Wiki iliyopita klabu ya Mtibwa ilimpa heshima mchezaji wao huyo wa zamani kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wao dhidi ya Lipuli FC ambapo alitumia fursa hiyo kuomba msaada ili aweze kupatiwa matibabu ya maradhi yanayomsumbua.

Baadhi ya wachezaji wa zamani na wa  sasa waliguswa na tatizo linalomsumbua mwenzao na kuamua kuchangishana fedha ili aweze kupatiwa matibabu ambapo wamewezesha kuanza kwa matibabu hayo.

Related Posts
1 of 980

“Tukiwa kama wachezaji tuliamua kuchangishana fedha ili tuweze kumsaidia mwenzetu, kwa bahati nzuri tumeweza kuwasiliana na wenzetu walioko nje ya nchi na wao wamechangia tumepata fedha ya kumuanzishia matibabu, ” alisema Salum Sued.

Vilevile Msemaji wa Mtibwa Thobias Kifaru amekipongeza kituo cha Azam TV kwa kuripoti tatizo la Modest hali iliyopelekea kumfikisha mchezaji huyo Dar kwajili ya matibabu huku pia akiiomba TFF pamoja na serikal ya awamu ya tano waweze kumsaidia ili aendelee na matibabu.

“Wachezaji peke yao hawana nguvu ya kumsaidia Alphonce kwa maumivu aliyonayo, nawaomba TFF pamoja na serikali waweze kumsaidia naamin Serikali ya awamu ya tano iko makini na naamini suala la Alphonce litachukuliwa kwa uzito”

Alphonce ameanza kufanyiwa vipimo jana na zeozi hilo limeendelea leo ili waweze kubaini tatizo linalomsumbua.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...