The sports Hub

AUSSEMS: Al Ahly Wakija ‘Kichwa Kichwa’ Watakula Nyingi Taifa

0 33

JOTO la pambano la Ligi ya Mabingwa Afrika likizidi kuongezeka, kocha wa Simba Mbeligiji Patrick Aussems, amewapa maneno ya ‘kuwatia ndimu’ wachezaji wake yenye lengo la kuhamasisha ushindi.

Aussems alisema kuelekea mechi ya kesho dhidi ya Al Ahly amefanya kazi ya kuwapa mbinu wachezaji za kuwakabili wapinzani, lakini wanapokuwa ndani ya uwanja linabakia kuwa ni jukumu la wachezaji kutekeleza majukumu yao.

“Wachezaji wangu wapo kwenye hali nzuri, najua wengi wanauzungumzia mchezo na Al Ahly kwa mitazamo tofauti tofauti, ila nikiwa kama kocha kwangu nafanya kazi yangu na nawaamini wachezaji wangu wataifanya kazi yao vizuri,” alisema Aussems.

Pia, kocha huyo amewataka wachezaji wake kuelekeza akili na mawazo yao kwenye mchezo huo ili waweze kufanya vizuri na kusahau kipigo cha mabao 5-0 walichokipata kutoka kwa Waarabu hao nchini Misri.

 

 

Get real time updates directly on you device, subscribe now.