The sports Hub

Aussems Awapigia Magoti Mashabiki Simba

0 119

BAADA ya kula vyema kiporo chake cha Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuibamiza mabao 3-0 Mwadui ya Shinyanga, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amewapoza wapenzi wa timu hiyo na kuwataka kutokata tamaa kwani bado wana nafasi ya kufanya vizuri katika Ligi ya Mabingwa wa Afrika.

Jumanne ya wiki ijayo, Simba itakuwa na mtihani mwingine wa kupata matokeo mbele ya Al Ahly ya Misri huku ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa mabao 5-0 na Waarabu hao katika mechi iliyopita.

“Niwaambie tu mashabiki na wapenzi wa timu ya Simba waendelee kuiunga mkono timu yao na wasikate tamaa baada ya kupoteza michezo miwili ugenini, bado tuna nafasi kwani michezo miwili ya hapa nyumbani naamini tutafanya vizuri,” alisema kocha huyo.

Alisema katika mechi mbili za ugenini ambazo wameruhusu mabao 10, ametambua matatizo ya timu yao na anayafanyia kazi hivyo timu hiyo itakuwa vizuri na wataondoka na pointi zote sita kutoka katika mechi mbili zilizobaki ambazo watachezea kwenye Uwanja waTaifa huku moja iliyobaki ikitarajiwa kupigwa ugenini.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.