Kitaifa

Baada ya Aveva Kaburu Kushikiliwa, Kamati ya Utendaji Simba Kukutana Kesho

on

KAMATI ya Utendaji ya klabu ya Simba kesho Jumamosi itakutana kujadili juu ya uendeshwaji wa klabu hiyo kufuatia viongozi wao kushikiliwa na vyombo vya dola.

Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange ‘Kaburu’ walishindwa kupata dhamana jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutokana na mashitaka yanayowakabili ya kughushi nyaraka za klabu na utakatishaji pesa dola 300,000 ambazo ni zaidi ya Sh 600 milioni mwaka jana.

Kamati hiyo itaangalia jinsi ya kuingoza klabu katika kipindi hiki ambacho viongozi hao wapo mahabusu huku zoezi la usajili likiendelea ambapo wamepanga kutotetereka licha ya kutokuwepo kwao.

Kwa mujibu wa Katiba ya Simba ni kwamba endapo viongozi wote wa juu wakipatwa na matatizo basi Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ambaye ni wa kuchaguliwa mwenye uzoefu na umri mkubwa ndiye atakayekabidhiwa jukumu hilo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mtandao maalum wa klabu hiyo umewataka wapenzi, mashabiki na wanachama wao kutulia na kuwa na subira huku wakiandaa Mawakili wazuri kwa ajili ya kusimamia kesi ya viongozi wao. Aveva na Kaburu wanatarajiwa kupandishwa kizimbani Julai 13.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *