The sports Hub

Baada ya Cameroon ‘Kuchemka’, Hii Ndio Siku ya Kumfahamu Mwenyeji wa AFCON19

0 127

BAADA ya Cameroon kupoteza nafasi ya kuandaa fainali za michuano ya mataifa ya Afrika (AFCON 2019), shirikisho la kabumbu Afrika limetangaza Januari 9 kuwa ndio siku ya kumfahamu mwenyeji mpya.

Cameroon ilipokonywa nafasi ya kuandaa michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Juni 15 hadi Julai 13 baada ya kuonekana inachelewa kufanya maandalizi huku kukiwa na udhaifu mkubwa kwenye mambo mengi kiujumla.

Afrika Kusini na Morocco ni kati ya nchi zinazopewa nafasi kubwa ya kuwa wenyeji lakini Congo-Brazzaville nao wameonesha nia na matamanio ya kuandaa mashindano hayo.

Morocco waliopoteza nafasi ya kuandaa Kombe la Dunia 2026 wanaweza kuwa katika njia nyeupe zaidi kwani kitendo chao cha kuwa tayari kuandaa michuano hiyo mikubwa zaidi duniani kinaashiria hawahitaji maandalizi makubwa sana kuweza kuandaa AFCON.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.