The sports Hub

Baada ya Kukamata Bajaji ya Sportpesa, Mama wa Nyumbani Aamua Kurudi Shule

0 738

TIMU ya Shinda Zaidi na SportPesa imebahatika kumpata mshindi mwigine mwanamama akiwa ni mwanamke watatu kujishindia Bajaji kutoka jiji la Dar es Salaam safari hii ‘chombo’ kikitua Goba.

Katika droo ya 64 Petronila Sirinya aliibuka mshindi ambaye alibashiri na moja kwa moja kuingia kwenye droo ya Shinda Zaidi na SportPesa na kujishindia Bajaji Re kutoka SportPesa.

Petronila alisema alianza kushawishika kucheza na SportPesa baada ya kuona vile watu wengine wanashinda kwenye promosheni ya Shinda zaidi ndipo na yeye akachukua uamuzi wa kuanza kucheza na timu ya ushindi akiutafuta ushindi wake.

“Nimeufurahia ushindi huu sijawahi kushinda kabisa tena mimi ni mama wa nyumbani sikufikiri kama ningeshinda lakini Mungu kanisaidia sasa nitaweza kumudu mahitaji yangu. Kutoka kukaaa nyumbani mpaka kumiliki bajaji yangu hizi ni baraka kubwa sana kutoka kwenu SportPesa,” alisema Petronila.

Aidha Petronila alisema kipato atakachopata kupitia bajaj hiyo kitamsaidia kujiendeleza kielimu zaidi huku pesa nyingine ataziwekea mipango mizuri kumuwezesha mtoto kusoma shule nzuri.

Maisha ya Petronila yalivyobadilika

“Najua hata mume wangu atakuwa ameshawishika sasa maana wakati nacheza alikuwa ananiambia shauri yako unapoteza pesa zako lakini baada ya kushinda yeye ndio ananisisitiza niendelee kucheza kweli ushindi una raha yake, ” alisema Bi. Sirinya.

Upande mwingine aliipongeza SportPesa kwa kutoa huduma bora kwa wateja wake sambamba na kuwajali kwa kuwatumia pesa za ushindi mara baada tu ya mechi kumalizia, huku akiweka wazi mikakati yake ya kuanza kusaka mtonyo wa Jackpot.

Kutoka SportPesa, Meneja Uhusiano Bi. Sabrina H. Msuya alisema kampuni hiyo ina huduma mbalimbali ambazo mteja akicheza anaweza kujishindia pesa ambazo anapata mara baada ya kuweka ubashiri wake na kupatia kiusahihi. Zawadi nyingine zitolewazo ni Bajaji , Simu janja pamoja na Jezi orijino za Simba na Yanga.

“Wiki hii Jackpot yetu imepanda mpaka shilingi 403,525,820/= ambapo mteja akibashiri kwa usahihi mechi kumi na tatu anaweza kuibuka na kitita hicho huku wale watakaobashiri kwa usahihi kuanzia mechi kumi hadi kumi na mbili watapata bonasi.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.