Kitaifa

Baada ya Kutua Singida, Atupele Afunguka Kuhusu Pluijm

on

BAADA ya kutua Singida United mshambuliaji Atupele Green amefunguka kuwa uwepo wa kocha Mholanzi Hans van Pluijm kwenye timu hiyo ni kitu ambacho kimechangia kutofikiria mara mbili kujiunga nao.

Atupele amesaini mkataba wa miaka miwili ambapo kwa sasa anaendelea na mazoezi na timu hiyo katika uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kujiwinda na michuano mipya ya SportPesa Super Cup itakayoanza Juni 5 katika dimba hilo.

Atupele ameiambia BOIPLUS kuwa alikuwa anatamani kufanya kazi na kocha Hans kwakua ni kocha mkubwa mwenye uzoefu ambaye atamuongezea vitu vingi na kumfanya awe bora zaidi msimu ujao.

Hans Pluijm siku alipotambulishwa rasmi Singida United

Atupele alisema msimu uliomalizika wiki mbili zilizopita haukuwa mzuri kwake ambapo timu yake aliyokuwa akiitumikia JKT Ruvu ilishuka daraja ikiburuza mkia huku kasi yake ya kucheka na nyavu ikipungua ila amejipanga ‘kukinukisha’ baada ya kuanza kwa msimu mpya mwezi Agosti.

“Kwa sasa nipo Singida United Chini ya kocha Pluijm, nilikuwa natamani kucheza chini yake namshukuru Mungu lengo langu limetimia.

“msimu ulioisha haukuwa mzuri kwangu na inatokea kwa mchezaji yoyote ila nimejipanga kufanya makubwa msimu ujao na Mungu atanisaidia.”

Atupele anakuwa mchezaji wa pili wa hapa nchini kujiunga na Singida baada ya nahodha wa Mbeya City Kenny Ally kufanya hivyo wiki iliyopita.

Mfungaji huyo bora wa kombe la FA wa mwaka jana anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kwenye michuano ya SportPesa itakayoanza wiki ijayo.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *