The sports Hub

Baada ya Kuwavimbia Mbao, Alliance Watua Dar Kuivaa African Lyon

0 58

TIMU ya Alliance FC imefika salama jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu hapo kesho dhidi ya African Lyon utakaochezwa katika uwanja wa Uhuru kuanzia saa 10:00 Alasiri.

Kikosi hicho kinachojengwa zaidi na vijana wadogo, Jumamosi iliyopita kilipambana kupata sare ya bila magoli katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania dhidi ya Mbao FC unaofahamika zaidi kama ‘Rock City Derby’.

Timu imefanya mazoezi asubuhi ya leo katika uwanja huo ambao utatumika kwa mchezo wa kesho kama kanuni zinavyoeleza.

Kwa mujibu wa mkuu wa idara ya habari na Mawasiliano, Jackson Mwafulango, timu hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya GF Trucks & Equipment itamkosa Michael Chinedu ambaye ni mgonjwa pamoja na Juma Nyangi na Wema Sadock wenye kadi tatu za njano kila mmoja.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.