Kitaifa

Baada ya Simba Kuipiga ‘Hattrick’ Azam, Yanga Waamua Kununua Ugomvi

on

NI wiki yenye mambo mengi katika medani ya soka hasa kutokana na vigogo kuingia kwenye vita ya usajili kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu na michuano ya kimataifa.

Simba wamefanikiwa kusajili nyota watatu (hattrick) toka Azam FC ambao ni John Bocco, Aishi Manula na Shomari Kapombe sambamba na mabeki Yusuf Mlipili (Toto African) na Jamal Mwambeleko (Mbao FC).

Wakati wekundu hao wakifanya yao na Azam wakiendelea kuimarisha kikosi kwa kusajili damu changa, mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Yanga wenyewe bado wapo kimya huku habari zikipasha kuwa mambo ya pesa bado hayajakaa sawa.

BOIPLUS ilijipenyeza hadi ndani ya ‘mjengo’ wa Wanajangwani hao kutaka kujua nini hasa siri ya ukimya wao ndipo ilipotoka kauli ambayo hakuna mwanasimba anaweza kuifurahia.

Chanzo chetu ndani ya klabu hiyo kongwe kilisema wao hawana haraka kwani wanafanya mambo yao kisayansi na mwisho wa siku watawanyamazisha wote wanaopiga kelele.

“Dirisha la usajili bado halijafunguliwa, nashangaa kusikia watu wameanza kusema Yanga itaambulia magalasa, sisi hatujawahi kufeli kwenye usajili, wachezaji wote tunaowahitaji tuko nao pazuri.

“Waambie hao majirani (Simba) kuna nyota watatu hawawezi kuwazuia kutua Jangwani na hapo ndipo watakapoelewa kimya chetu kina maana gani,”. Alisema kiongozi huyo kwa sharti la kutotajwa jina mtandaoni.

Alipoulizwa kuhusu majina ya nyota hao kiongozi huyo alisema hawezi kuwataja kwavile bado kuna mambo machache hayajakamilika huku akiahidi kupiga simu kwenye ofisi za BOIPLUS mara mambo yatakapokaa sawa.

Hata hivyo mtandao huu unafahamu kuwa nyota watatu wanaowaniwa na Yanga ni Jonas Mkude, Ibrahim Ajibu na Said Ndemla ingawa Wekundu wa Msimbazi wanapambana kuhakikisha wanabaki nao msimu ujao.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *