Kimataifa

Baada ya Ujerumani na Chile Kufuzu, Hapatoshi Nusu Fainali Mabara

on

MOSCOW, Urusi
TIMU za Ujerumani na Chile zimeungana na Ureno pamoja na Mexico kutinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la mabara baada ya kumaliza vinara katika kundi B.

Ujerumani iliibugiza Cameroon mabao 3-1 huku Chile ikilazimishwa sare ya bao moja na Australia na kutinga katika hatua hiyo.

Ujerumani imemaliza kinara wa kundi hilo ikiwa na pointi saba huku Chile ikiwa na pointi tano katika nafasi ya pili wakati Cameroon na Australia zikiaga mashindano hayo.

Hii ina maana kuwa Ujerumani ambaye ni kinara wa kundi B atacheza na Mexico aliyemaliza nafasi ya pili kundi A huku Ureno akimenyana na Chile.

Nusu fainali ya kwanza itakuwa kati ya Ureno dhidi ya Chile Juni 28 wakati ile ya pili ikifanyika siku moja baadae.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *