Kitaifa

Bado wanne tu mziki ukamilike Jangwani

on

WACHEZAJI wanne pekee ndio bado hawajajiunga na kambi ya mabingwa watetezi wa ligi ya Tanzania bara timu ya Yanga iliyopo mkoani Morogoro ili kukamilisha ‘mziki’ kamili kuelekea msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom.

Wachezaji hao ni Donald Ngoma na Thaban Kamusoko ambao wanatarajia kujiunga na wenzao muda wowote kuanzia sasa huku Hassan Kessy akipewa mapumziko mafupi baada ya kutoka kwenye majukumu ya timu ya taifa wakati mlinda mlango Benno Kakolanya akiwa bado hayuko fiti kutokana na kuwa majeruhi.

Kikosi hicho ambacho kipo chini ya kocha mkuu George Lwandamina na msaidizi wake Noel Mwandila kiliwasili mkoani humo kwa kambi ya siku 10 juzi usiku ambapo walifanya mazoezi asubuhi na jioni ya jana.

Makamu mkuu wa kitengo cha Habari na mawasiliano cha klabu hiyo Godlisten Anderson ‘Chicharito’ ameiambia BOIPLUS kuwa wachezaji wote wapo katika hali nzuri wakipokea mafunzo kutoka kwa makocha wao.

Thaban Kamusoko atawasili kambini Morogoro muda wowote akiwa na Donald Ngoma

“Kikosi kizima cha Yanga kipo huku isipokuwa wachezaji wanne tu ambao wote uongozi una taarifa zao za kushindwa kujiunga na wenzao kambini. Wachezaji hao ni Ngoma, Kamusoko, Kessi na Kakolanya ila kiujumla kambi inaendelea vizuri na wachezaji wapo katika hali nzuri pia,” alisema Chicharito.

Yanga itarejea jijini Dar es Salaam siku chache kabla ya kukutana na Singida United katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika kwenye uwanja wa Taifa, Agosti 6.

Baada ya mchezo huo Yanga itashuka tena dimbani Agosti 23 kucheza na watani wao Simba katika mechi ya ngao ya hisani kuashiria kufunguliwa kwa pazia la ligi kuu ya Vodacom.

Wakati huo huo kikosi cha vijana cha Yanga (U20) jana kimeishushia kichapo cha mabao 3-0 Mbeya City kwenye mchezo maalum wa kirafiki ulioandaliwa na tume ya kudhibiti UKIMWI, TACAIDS.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *