Kitaifa

Blagnon Ndiye ‘Kikongwe’ Zaidi Msimbazi

on

STRAIKA wa Simba, Fredrick Blagnon raia wa Ivory Coast ndiye mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi katika kikosi hicho kilichocheza mechi ya Sportpesa Super Cup dhidi ya Nakuru All Stars ya Kenya. Mechi hiyo imechezwa uwanja wa Uhuru.

Blagnon ambaye alikaa benchi akisubiri kufanyiwa mabadiliko aliwazidi wachezaji wote kwani katika kikosi hicho imeonyesha kuwa alizaliwa Disemba 24, 1985 akifuatiwa na kiungo Mwinyi Kazimoto aliyezaliwa Desemba 25, 1988.

Wengine ambao ni wadogo zake Blagnon ni Janvier Bokungu, Vincent Costa na Daniel Agyei waliozaliwa mwaka 1989 ingawa wametofautiana miezi na tarehe za kuzaliwa huku wengine ikionesha kuwa walizaliwa kuanzia miaka ya 1990. Mohamed Musa ndiye kinda kuliko wote kwani amezaliwa Machi 07, 1999.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Sheila Ally

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *