Kitaifa

Bokungu mapicha picha tu Simba, haelewi kitu

on

Akram Msangi

BEKI wa kulia wa Simba, Mkongomani Javier Bokungu ameshangazwa na uongozi wa Wekundu hao kutomwambia chochote kuhusu mustakabali wake ndani ya kikosi hicho.

Mkataba wa Bokungu na Simba unamalizika Agosti 6 lakini mpaka sasa hakuna kiongozi yeyote aliyempigia kuhusu kujiunga kambini na wenzake au kuambiwa kama ameachwa ili atafute timu nyingine.

Akizungumza na BOIPLUS akiwa mapumzikoni nchini Kongo, Bokungu alisema mpaka sasa haelewi chochote kuhusu mustakabali wake ndani ya Simba kwakua hajapewa taarifa rasmi kama ameachwa au la.

“Mkataba wangu na Simba unamaliza Agosti 6, lakini mpaka sasa sielewi chochote sababu hakuna kiongozi aliniyenipa taarifa ya aidha kuachwa au nitaendelea kuwepo,” alisema Bokungu.

Mchezaji huyo wazamani wa TP Mazembe amesema hapendi kucheza soka nchini Kongo hivyo atatafuta timu nje hata kama atakuwa ameachwa na mabingwa hao wa kombe la FA.

BOIPLUS inafahamu kuwa beki huyo na wachezaji Fredrick Blagnon na Daniel Agyei ni miongoni mwa wachezaji wa kimataifa ambao hawana nafasi ya kuendelea kuchezea Simba msimu ujao.

Wachezaji wa kimataifa ambao watachezea Simba msimu ujao ni pamoja na Juuko Murshid, Laudit Mavugo, Emmanuel Okwi, Method Mwanjale, James Kotei, Nicholas Gyan na Haruna Niyonzima ambaye bado usajili wake haujakamilika mpaka sasa.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *