Kimataifa

Bravo ‘Aficha’ Penati Tatu na Kugeuka Shujaa

on

MOSCOW, Urusi
MLINDA mlango Claudio Bravo ameibuka shujaa wa nchi yake ya Chile baada ya kuokoa mikwaju mitatu ya penati katika ushindi wa penati 3-0 dhidi ya Ureno kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya michuano ya kombe la mabara inayoendelea nchini Urusi.

Bravo ambaye anachezea klabu ya Manchester City ya Uingereza alionyesha kujiamini langoni pake na kufanikiwa kuwazuia Ureno wasifunge penati yoyote huku wachezaji wake wakifunga zote tatu na kufanikiwa kutinga fainali ya michuano hiyo.

Mchezo huo ulilazimika kwenda katika hatua hiyo baada ya kumalizika kwa sare ya bila kufangana kwenye muda wa kawaida na dakika 30 za nyongeza.

 

Ureno walicheza vizuri wakimiliki mchezo kwa kiasi kikubwa huku Chile wao wakifanya mashambulizi machache makali ya kushtukiza.

Penati za Chile zilifungwa na Arturo Vidal, Alexis Sanchez na Fernandez huku Ricardo Quaresma, Joao Moutinho na Luis Nani wakikosa kwa upande Ureno.

Mchezo mwingine wa nusu fainali utachezwa Alhamisi hii kati ya Ujerumani dhidi ya Mexico.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *