Afrika

BWALYA: Simba Kama Mkwanja Upo Njooni

on

Straika Walter Bwalya anayekipiga katika klabu ya Nkana Rangers amesema kuwa yupo tayari kutua Simba kama wataweza kumpa donge nono la usajili na Si vinginevyo.

Simba wameweka kwenye faili lao la usajili jina la Bwalya ambaye ndiye kinara wa mabao nchini Zambia lakini wanaumiza kichwa jinsi ya kuvunja benki kwa ajili ya kumnunua nyota huyo.

Bwalya ameiambia BOIPLUS kuwa yeye hachagui wapi acheze lakini anachoangalia zaidi ni maslahi atakayoyapata kwa wakati huo.

“Mimi nina wakala wangu ingawa nilipigiwa simu na nmoja wa watu kutoka Simba, naweza kuja kama wataweza kunilipa kwani mimi nacheza popote ili mradi tufikie makubaliano mazuri,” alisema Bwalya kutokea Zambia.

Simba itawaacha baadhi ya nyota wao  kigeni ambapo Daniel Agyei, Frederick Blagnon na Janvier Bokungu wanatajwa kuwemo kwenye orodha ya watakaotemwa.

Mpaka sasa wenye uhakika wa kuwemo kwenye kikosi kipya ni Emmanuel Okwi, James Kotei, Juuko Murshid, Method Mwanjali Laudit Mavugo. Hivyo bado nafasi mbili za wachezaji wa kigeni kujazwa.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Sheila Ally

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *