The sports Hub

CAF Yamsukuma Ndani Mwamuzi wa Fainali ya Mabingwa

0 130

SHIRIKISHO la soka barani Afrika(CAF), limemsimamisha kutojihusisha na shughuli zozote za soka zilizopo chini ya CAF mwamuzi Mehd Abid Charef baada ya kuboronga katika fainali ya Ligi Mabingwa Afrika.

Charef alikuwa mwamuzi katika mechi ya fainali ya mkondo wa kwanza wa klabu bingwa kati ya Al Ahly na Esperance uliopigwa jijini Alexandria nchini Misri.

Katika fainali hiyo Al Ahly waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 ambapo Charef aliwazawadia penati mbili na mabingwa hao wa Misri kushinda mchezo huo uliogubikwa na maamuzi tata. Bao la Esperance pia lilitokana na mkwaju wa penati.

CAF walitumia mfumo wa video na kujiridhisha kuwa Charef alitoa upendeleo kwa timu ya Al Alhy na kuacha kutoa adhabu kwa baadhi ya makosa katika mchezo huo hivyo atalazimika kukaa pembeni hadi kamati itakapotoa maamuzi ya shauri lake la madai ya rushwa.

Charef anakuwa mwamuzi mwingine mzoefu ‘kusukumwa ndani’ baada ya CAF kumfungia aliyekuwa mwamuzi kutoka Zambia Janny Sikwaze kwa sababu ambazo zinafanana na Charef.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.