Kimataifa

Cameroon ‘Chali’ Mabara, Wakubali Kichapo Toka Chile

on

MOSCOW, Urusi
CHILE imeanza vyema michuano ya Kombe la Mabara iliyoingia siku ya pili leo baada ya kuifunga Cameroon mabao 2-0 katika mchezo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa.

Dakika ya 45 Edward Vagas alifunga bao baada ya kumalizia pasi ya Artulo Vidal lakini lilikataliwa na mwamuzi baada ya picha za video kuonyesha mshambuliaji huyo alikuwa ameotea.

Alexis Sanchez aliyetokea benchi alifanya kazi ya kutengeneza bao la kwanza lililofungwa na Vidal dakika ya 81 baada ya kupiga krosi safi iliyomaliziwa kwa kichwa na kiungo huyo wa Bayern Munich.

Sanchez tena aliwalamba chenga  walinzi wa Cameroon na mlinda mlango wao Ondoa kisha kupiga shuti lililozuiwa kabla ya kumkuta Vargas ambaye alifunga kirahisi dakika ya 90.

Katika mchezo wa awali wa kundi A, Ureno ilitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Mexico.

Kesho kutakuwa na mchezo mmoja wa kundi B kati ya Australia dhidi ya Ujerumani.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *