The sports Hub

CHAMA: Nimepata Wakati Mgumu Sana

0 1,984
Bonyeza picha hii hapa juu kujisajili na kucheza

KIUNGO wa Simba Clatous Chama amesema ni jambo la furaha kwake  kuipeleka timu hatua ya makundi ya Kombe la Mabingwa barani Afrika lakini hatosahau aliyokutana nayo katika dakika 180.

 

Akizungumza na BOIPLUS MEDIA mara baada ya kumalizika kwa pambano hilo, Chama alisema kila mmoja katika timu amefurahi sana kwani haikuwa rahisi ila kwa upande wake hali ilikuwa ngumu zaidi kwani alikuwa anacheza na watu wanaomfahamu vizuri.

“Kucheza na watu wanaokufahamu vema mtindo wako ni ngumu sana, nimepata wakati mgumu katika mechi zote mbili, kama ulivyoona kila nikigusa mpira walikuwa wakija kwa pamoja lakini nashukuru tu mwisho nimeisaidia timu yangu,” alisema Chama.

 

Simba imefanikiwa kutinga hatua ya makundi baada ya kuifunga Nkana kwa jumla ya mabao 4-3 ikishinda mabao 3-1 kwenye dimba la taifa yaliyoizima Nkana ambayo ilikuwa na matumaini kutokana na ushindi wao wa mabao 2-1 nyumbani kwa Zambia.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.