Kitaifa

‘Chui’ Waitemesha Mzigo Yanga

on

TIMU ya AFC Leopards imekuwa ya kwanza kutinga fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penati 4-2 mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Matokeo hayo yamefanya timu zote nne kutoka Tanzania zilizokuwa zikishiriki michuano hiyo kuondolewa kwenye michuano hiyo na kuwaacha Wakenya kutawala. Timu hizo ni Simba,Yanga, Jang’ombe Boys na Singida United.

Mchezo huo ulikosa msisimko hasa kipindi cha kwanza kutokana na timu zote kucheza taratibu huku kukiwa na mashambulizi machache pande zote na kupelekea mtanange kumalizika bila kufungana.

Juma Mahadhi wa Yanga akijaribu kuwatoka walinzi wa AFC Leopards

Yanga iliingia katika mchezo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuitoa Tusker kwa mikwaju ya penati huku Leopards pia ikiwatoa Singida United kwa staili hiyo.

Kocha Juma Mwambusi wa Yanga aliwatoa Emmanuel Martin, Yusuph Mhilu, Pato Ngonyani na Maka Edward nafasi zao zikachukuliwa na Said Mussa, Samwel Greyson, Said Makapu na Babu Ally wakati Leopards iliwatoa Gilbert Fiamenyo na Marcus Abwao na kuwaingiza Marselas Ingotsi na Mike Kibwage.

Wachezaji Benard Mango, Alan Kateregga, Vincent Oburu na Jan Otieno walifunga penati zao kwa upande wa Leopards wakati Marslelas Ingotsi akikosa mkwaju wake na upande wa Yanga Nadir Haroub na Obrey Chirwa walifunga kwa Yanga Huku Said Makapu na Said Mussa.

Gor Mahia iliyoibamiza Nakuru All Stars mabao 2-0 itacheza fainali na Leopards Jumapili katika uwanja huo.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *