Kitaifa

Chuji, Boban Wamduwaza Wanyama Ndondo Cup

on

WACHEZAJI wakongwe Haruna Moshi ‘Boban’ na Athuman Idd ‘Chuji’ wameonyesha uwezo mkubwa na kuiongoza timu ya Faru Jeuri kushinda bao moja dhidi ya Kauzu FC katika michuano ya Ndondo Cup iliyoshuhudiwa na kiungo wa Tottenham Victor Wanyama kwenye uwanja wa Kinesi.

Nyota hao wa zamani wa timu za Simba na Yanga walicheza kwa dakika zote 90 huku wakionyesha umahiri mkubwa mbele ya vijana katika idara ya kiungo hali iliyomfanya kiungo huyo mkenya ashindwe kuzuia hisia zake kwa burudani aliyokuwa akiishuhudia.

Wachezaji wa Faru Jeuri wakishangilia bao lao pekee katika mchezo huo

Tumba Swedi ambaye anachezea Mbeya City aliipatia Faru bao hilo pekee dakika ya 45 baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Kauzu.

Kauzu ambao waliongozwa na nahodha Godfrey Taita walirudi kwa kasi kipindi cha pili kwa kufanya mashambulizi langoni kwa Faru lakini hawakuweza kurudisha bao hilo.

Swedi angeweza kufunga mabao mengine kama angeongeza umakini baada ya kupoteza nafasi za wazi kadhaa akiwa anatazamana na mlinda mlango wa Kauzu.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *