The sports Hub

Coastal Union yaipiga mkwara mzito Simba

0 11

WAKATI Coastal Union wakijitupa katika Uwanja wao wa Mkwakwani, Tanga kesho saa 8 mchana kuwakabili Simba, kocha Juma Mgunda ameibuka na kudai kuwa kwa sasa hana tena masihara katika mechi yoyote hivyo timu hiyo ijipange.

Mgunda ambaye ni kocha mzoefu katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara, alisema amewapanga vijana wake vizuri kuhakikisha wanashinda mchezo huo ili kuzidi kujikusanyia pointi.

“Kwetu sisi tumejipanga vizuri kuhakikisha tunapata matokeo mazuri michezo yetu yote, sio huu wa Simba bali yote ndiyo maana tumekuwa tukifanya maandalizi mazuri,” alisema.

Coastal Union ipo nafasi ya nane baada ya

kucheza michezo 32 ikiwa imejikusanyia pointi 41 huku Simba wakiwa wamecheza michezo 22 wana poiti 57 wakiwa nafasi ya tatu.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.