The sports Hub

DANGOTE: Kama Arsenal ‘Wanazingua’ Nitanunua Klabu Nyingine

0 545

TAJIRI nambari moja Afrika, Aliko Dangote ambaye aliwahi kutangaza nia ya kuinunua klabu ya Arsenal ya Uingereza, amesema atabadili mawazo na kutafuta timu nyingine ya kuinunua kama mmiliki wa Washika Bunduki hao, Stan Kroenke atashikilia msimamo wa kutoiuza.

Raia huyo wa Nigeria ambaye ni shabiki wa kutupwa wa Arsenal mwenye utajiri unaokadiriwa kufikia paundi 8.5 bilioni hajawahi kuficha nia yake ya kuwa mmiliki wa klabu hiyo ambapo katika matamshi yake ya karibuni alisema angeuanzisha mchakato huo rasmi baada ya kumaliza ujenzi wa mtambo wake mpya wa kusafisha mafuta jijini Lagos unaotajwa kuwa ni katika kitambo mikubwa zaidi duniani.

Dangote alianza kutangaza nia Agosti, 2017 kabla hajashindilia msumari Julai mwaka huu kwa kusema ‘atakiwasha’ tena 2020 baada ya kukamilika kwa mtambo wake huku akisisitiza jambo hilo halitoangalia kama kuna mtu mwingine atainunua au la.

Mmiliki wa Arsenal, Stan Kroenke (kushoto)

“Kama watatangaziwa dau zuri naamini wataamua kuiachia, inaweza kutokea mtu akawapa kinachoweza kuwashawishi kufanya maamuzi na wakaizua, ila nikimaliza mradi wangu tu nitaingia vitani kuhakikisha nainunua Arsenal,” alisema Dangote Julai.

Lakini akizungumza na Blomberg TV katika kongamano jipya la kiuchumi nchini Singapore, tajiri huyo mwenye umri wa miaka 61 amesema sasa atalazimika kuangalia timu mbadala kama Kroenke ataonyesha ugumu katika kuiachia Arsenal.

“Naipenda sana Arsenal lakini kama haiuzi sitakuwa na namna, nitatafuta klabu nyingine kwavile mimi ni shabiki wa soka, natamani siku moja nimiliki klabu hata kama isipokuwa Arsenal. Hadi tumalize mradi wetu tutakuwa na kipato cha paundi 22.8 bilioni,” alimaliza kwa kujinasibu ‘Taikuni’ huyo.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.