Kitaifa

DEAL DONE: Maajabu ya Singida United Yaendelea kwa Kenny Ally

on

HATIMAYE nahodha na kiungo wa timu ya Mbeya City Kenny Ally amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Singida United ambayo imedhamiria kufanya maajabu katika msimu mpya wa ligi utakaonza mwezi Agosti kutokana na usajili unaoendelea kufanyika klabuni hapo.

Jana mtandao huu wa BOIPLUS uliripoti kuhusu dili hilo kukamilika mapema leo hii kutokana na kiungo huyo kusafiri kuja jijini Dar es Salaam tayari kusaini mkataba na timu hiyo iliyopanda daraja msimu huu.

Taarifa hizo huenda zikawa mbaya kwa timu za Yanga na Azam ambazo zilikuwa zikihitaji saini ya kiungo huyo aliyekuwa kwenye kiwango bora na usiku wa kuamkia leo amechaguliwa katika kikosi bora cha msimu wa ligi kuu ya Vodacom 2016/17.

Kenny Ally akisaini mkataba na Singida United

Yanga ndio ilikuwa ya kwanza kuwania saini ya kiungo huyo ambapo walitakiwa kulipa sh 40 milioni lakini wakashindwa kutoa dau hilo kabla ya Azam kufanya nae mazungumzo pia ila hawakufikia muafaka hadi leo aliposaini na Singida.

Singida inaonekana imepania kufanya vizuri msimu ujao wa ligi kutokana na usajili unaondelea tangu ilipofanikiwa kupanda ligi kuu zoezi likiongozwa na aliyekuwa kocha wa Yanga Mholanzi Hans van Pluijm ambaye ndiye atainoa hiyo msimu ujao.

Timu hiyo ni miongoni mwa timu tatu kutoka Tanzania zilizopata udhamini kutoka kwa kampuni ya michezo ya bahati nasibu SportPesa ambapo kwa mwaka itachukua kiasi cha shilingi milioni 250 ambazo inazifanya timu nyingine kuanza kuitazama kwa jicho la tatu.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *