Kitaifa

DEAL DONE: Raphael Daud atulizwa Jangwani

on

BAADA ya tetesi za muda mrefu hatimaye mabingwa watetezi wa ligi ya Vodacom timu ya Yanga wamekamilisha usajili wa kiungo Raphael Daudi kutoka Mbeya City kwa mkataba wa miaka miwili.

Yanga wamekuwa wakihusishwa na kiungo huyo fundi kwa muda mrefu hadi leo walipokamilisha ‘deal’ huku akitajwa kuziba pengo la Haruna Niyonzima ambaye amesajiliwa na Simba.

Kamati ya usajili ya klabu hiyo chini ya Mwenyekiti wake Hussein Nyika imekuwa ikifanya kazi kwa usiri mkubwa na leo wamekamilisha usajili wa kiungo huyo ambaye anatarajiwa kujiunga na wenzake waliopo kambini mjini Morogoro muda wowote kutoka sasa.

Uwezo mkubwa aliouonyesha kiungo huyo msimu uliopita ulisababisha kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Salum Mayanga kumjumuisha kwenye kikosi kilichoshiriki michuano ya COSAFA iliyofanyika nchini Afrika Kusini.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *