The sports Hub

DJUMA: Simba wanaweza kufanya kweli DR Congo

0 33

Aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Simba SC, Mrundi Irambona Masoud Djuma ameitabiria makubwa klabu ya Simba katika mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo, utakaochezwa Jumamosi jijini Lumbumbashi. 

Djuma amesema pamoja na Simba kupata sare katika uwanja wa nyumbani lakini ana imani kubwa kuwa wataweza kufanya vizuri wakiwa ugenini kutokana na kuwa na wachezaji wa kiwango cha juu wanaoweza kupamba na timu yoyote.

“Kweli TP Mazembe ni timu ngumu na kongwe. Ukiangalia ina historia kubwa Afrika na ndani ya miaka hii kumi tumeshuhudia ikitwaa ubingwa tofauti wa michuano ya CAF mara tano. Ni rekodi bora sana lakini pamoja na ubora wao nikiangalia ubora na uthubutu wa wachezaji wa Simba, naona wanaweza kufanya kweli,’’ alisema.

Mrundi huyo aliongeza kwa kusema kitu pekee

kinachopaswa kufanywa na wachezaji na viongozi wa Simba ni kutokuwa na wasiwasi na  mchezo huo na badala yake kuelekeza nguvu na akili zao uwanjani.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.