Kitaifa

Dstv wazindua msimu mpya wa ligi kivingine

on

KAMPUNI ya Multichoice (Dstv) kupitia kituo chake cha Supersport imezindua msimu mpya wa soka uliopewa jina la ‘Full Vyenga Bila Chenga’ kuelekea msimu mpya wa ligi kuu mbalimbali kote duniani.

Supersport imekuwa ikionyesha ligi maarufu duniani kama ya Uingereza, Hispania, Ujerumani, Ufaransa na Italia na kufanya mashabiki wengi wa soka sehemu mbalimbali kufuatilia michezo hiyo.

Mkurugenzi wa Dstv, Maharage Chande amesema msimu huu wa ligi wamejipanga kuonyesha mechi zote za ligi hizo tena kwa muonekano ang’avu ‘high definition’ ili kuwafanya mashabiki kuwaona wachezaji kama walivyo huku wakishusha bei ya gharama zao.

“Tumejipanga kuonyesha mechi za ligi zote maarufu duniani kwa muonekano mzuri, tunawaomba wapenzi wa soka kulipia ving’amuzi vyao ili wasipitwe na burudani hizi na tunaanza rasmi mwishoni mwa wiki hii,” alisema Chande.

Kwa upande wake Ephraim Kibonde ambaye ni miongoni mwa watangazaji watakaorusha matangazo hayo kwa lugha ya kiswahili amesema mashabiki wa soka wategemee vitu vizuri kutokana na mipango thabiti iliyowekwa kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa ligi.

“Mashabiki waendelee kufuatilia matangazo ya ligi mbalimbali Ulaya kwa lugha ya Kiswahili ambapo watapata kwa muonekano mzuri na sauti zitaendana na matukio uwanjani,” alisema Kibonde.

Mbali na mtangazaji huyo nguli wa michezo wengine watakaotangaza kwa Kiswahili ni pamoja na Maulid Kitenge, Oscar Oscar na Ibrahim Masoud ‘Maestro’.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Akram Msangi

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *