Afrika

Dylan Kerr Kuanza na Everton Dar

on

NAIROBI, Kenya
MABINGWA wa ligi kuu nchini Kenya timu ya Gor Mahia wamemtangaza kocha wa Kimataifa raia wa Uingereza aliyewahi kuifundisha Simba ya jijini Dar, Dylan Kerr kuwa kocha wao mkuu na kwamba atajiunga na timu Julai 8 kabla haijatua Dar kupambana na Everton Julai 13.

Licha ya Simba, Kerr 49 amewahi kuifundisha timu ya Mpumalanda Black Aces ya Afrika Kusini na anatarajia kuchukua nafasi ya kocha Jose Marcelo Fereira ‘Ze Maria’ raia wa Brazil ambaye alitimka klabuni hapo wiki kadhaa zilizopita na kujiunga na timu ya FK Tirana ya Albania.

Kocha msaidizi Zedekiah Otieno ‘Zico’ anakaimu nafasi ya kocha mkuu ambapo katika michezo miwili ya ligi aliyosimamia amepoteza mmoja na kutoka sare wa pili. Zico ataendelea kuwa kocha msaidizi wakati Wilis Ochieng akiwa kocha wa magolikipa huku Jolawi Obondo akibaki katika nafasi yake ya Meneja wa timu.

Wachezaji wa Gor Mahia

Katika soka la kimataifa Kerr amewahi kuchezea timu za Uingereza ambazo ni, Sheffield United, Leeds United na Reading FC. Pia alichezea timu ya Arcadia Shepherds FC kutoka Afrika Kusini mwishoni mwa miaka ya 1980 kabla ya kutundika daruga.

Alianza kufundisha soka nchini Afrika Kusini akiwa kocha msaidizi katika klabu ya Mpumalanga Black Aces mwaka 2009 na baadae akajiunga na Thanda Royal Zulu na Nathi Lions. Pia alifundisha soka nchini Vietnam katika ngazi ya klabu na timu ya Taifa.

Akiwa Vietnam aliisaidia timu ya Hai Phong FC kutwaa taji la na kufuzu katika michuano ya klabu bingwa bara la Asia.
SOURCE: Futaa.Com

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *