Kitaifa

Everton watua Dar kama mabubu

on

KIKOSI cha Everton kimetua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Nyerere (JNIA) asubuhi ya leo na kuingia moja kwa moja kwenye basi lao bila kuzungumza chochote.

Kikosi hicho kinachodhaminiwa na kampuni ya SportPesa kimetua kwa ndege maalum majira ya saa 3 asubuhi kikiwa na nyota wote akiwemo straika wao aliyesajiliwa hivi karibuni, Wayne Rooney.

Kiu ya wanahabari wengi waliojitokeza uwanjani hapo ilikuwa ni kufanya mahojiano na nyota kadhaa wa timu hiyo lakini hakuna mchezaji wala kiongozi aliyezungumza chochote licha ya jitihada za Waziri mwenye dhamana ya michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kufanikisha azma hiyo.

Baada ya tukio hilo Waziri Mwakyembe alizungumza na wanahabari na kuwaeleza kuwa watapata muda wa kuzungumza na nahodha baadae kwa utaratibu utakaoelezwa.

Nyota hao wanatarajia kufanya mazoezi jioni ya leo kwenye uwanja wa taifa lakini hakuna shabiki wala mwandishi wa habari atakayeruhusiwa kuhudhuria.

“Tumezungumza nao, mtapata nafasi ya kufanya mahojiano na nahodha, leo watafanya mazoezi kwenye uwanja wa taifa lakini hakuna mtu ataruhusiwa kufika eneo lile, kutakuwa na ulinzi mkali,” alisema Mwakyembe.

Everton itapambana na Gor Mahia FC kesho kwenye uwanja huo wa taifa katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *