The sports Hub

Farid Mambo Si Mambo Hispania, Adhamiria Kuvunja Mkataba

0 500

MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Tanzania anayeitumikia Klabu ya CD Tenerife inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza nchini Hispania Farid Mussa amesema anatazamia kuvunja mkataba na timu hiyo kutokana na kukosa namba ndani ya kikosi hicho.

Farid ambaye aliitumikia Klabu ya Azam FC kabla ya kutolewa kwa mkopo Tenerife na baadaye kununuliwa moja kwa mojnna,  amesema, mara baada ya kuona anakosa nafasi aliuomba uongozi wa Klabu hiyo umtoe hata kwa mkopo lakini ulikataa na hata timu nyingine zilipomuhitaji zilikataliwa kwa madai kuwa wanampango naye kwa msimu ujao.

“Unajua kipindi nilivyokuja hapa nilikubali kucheza ligi ya Tatu kwa huku nikifanya mazoezi na timu kubwa na nikafanikiwa kuwapa ubingwa wa Segunda ambayo anacheza Shaban Idd sasa hivi kwa mkopo, Timu nyingi kwa sasa zinanihitaji baada ya kuona sipati namba lakini uongozi wa Tenerife unakataa kwa maelezokuwa bado wanamipango na mimi,” amesema Farid.

Farid Mussa

Farid ameongeza kuwa aliwaomba atolewe kwa mkopo pia wakakataa. Tenerife hawakuona hatari kukataa pia ofa ya Extemadura FC ambao walitaka kukaa mezani ili wamnunue moja kwa moja.

“Hapa kilichopo ni kusubiria mkataba uishe mwishoni mwa mwaka huu kwa maana hamna namna  kama itaendelea hivi wakala wangu amesema itabidi  tuvunje mkataba. Nashindwa hata kuwaelewa na kuna muda nakosa hata raha,” amesema Farid.

Farid alijiunga na Tenerife Disemba 2016 kwa mkopo wa muda mrefu wa msimu mzima kutoka Azam kwa makubaliano maalum baada ya winga huyo kufuzu majaribio katika klabu hiyo na baada ya kutua Tenerife akapangiwa kuanza kuchezea kikosi cha U20 ili kupata uzoefu kabla kupandishwa kikosi cha kwanza kinachocheza.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.