The sports Hub

Fei Toto Aahidi Kufuata Nyayo Za Samatta

0 26

KIUNGO wa Yanga, Feisal Salum ‘Fei Toto,’  amesema ndoto yake kubwa katika soka ni kutaka kufikia anga alizofikia nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta.

Fei Toto alifichua kuwa ana ndoto ya kucheza nje ya nchi kama ilivyokuwa kwa Samatta anaichezea klabu ya Genk ya Ubelgiji baada ya kutamba na Simba na TP Mazembe ya DR Congo.

“Mimi binafsi natamani mafanikio ya Samatta, ametuonyesha njia na kwangu natamani kufikia alipofika yeye. Hakuna mchezaji ambaye hapendi mafanikio makubwa ya kucheza nje ya nchi,” alisema Fei Toto.

Alisema anajituma ili kuweza kulinda kiwango chake cha sasa na hatimaye kutimiza ndoto yake hiyo. Hivyo basi, atatumia upenyo alioupata Yanga ili kuweza kutimiza malengo yake ya kufika mbali.

 

Get real time updates directly on you device, subscribe now.