Kimataifa

Genk waanza kwa sare Samatta akitupia nyavuni

on

LICHA ya straika Mbwana Samatta kuisawazishia KRC Genk na baadae Trossard kuipatia bao la kuongoza bado kikosi hicho kilishindwa kuibuka na pointi tatu baada ya kulazimishwa sare ya mabao matatu na Waasland-Beveren nyumbani.

Wageni Beveren walikuwa wa kwanza kupata bao katika uwanja wa Luminus Arena lililowekwa nyavuni na Oliver Myny dakika moja kabla ya mapumziko.

Straika Zinho Gano aliipatia Beveren bao la pili kabla Naranjo hajafungua ukurasa wa mabao kwa upande wa Genk dakika tatu tangu aingie kuchukua nafasi ya Ruslan Malinovsky.

Samatta aliipatia Genk bao la kusawazisha dakika ya 80 likifuatiwa na bao la tatu dakika mbili baadaye lililofungwa kiufundi na Trossard.

Ikionekana kama vile Genk wangeondoka na pointi zote tatu katika mchezo huo wa kwanza, Gano aliisawazishia Beveren dakika ya 90 na kuzifanya timu hizo kugawana pointi.

Samatta alicheza mechi ya jana akiwa na maumivu ya shingo aliyoyapata katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Everton juma lililopita.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *