Kitaifa

Gor Mahia Wawatuliza Mashemeji Zao na Kutwaa Mamilioni ya SportPesa

on

MICHUANO mipya ya SportPesa Super Cup imemalizika huku ikishuhudiwa Gor Mahia ikiibuka mabingwa kwa kuwafunga wapinzani wao wa jadi AFC Leopards mabao 3-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru.

Michuano hiyo ilianza Juni 5 ikishirikisha timu nane kutoka Tanzania na Kenya ambapo miamba hiyo ya Kenya ilifanikiwa kutinga fainali na kuziacha timu za nyumbani zikiwa watazamaji.

 

Katika mchezo huo uliopewa jina la ‘Mashemeji Derby’ ambao ndio unaovuta hisia za mashabiki wengi nchini Kenya ulianza taratibu kwa timu zote kushambuliana kwa zamu lakini hakuna aliyepata bao hadi wanaelekea mapumziko.

Kipindi cha pili Gor walirudi kwa kasi ambapo walifanikiwa kupata mabao katika dakika za 65, 80 na 90 kupitia kwa Timothy Otieno, Oliver Maloba na John Ndirangu.

Mshambuliaji wa Gor Medie Kagere ameibuka mfungaji bora wa michuano hiyo kwa kufunga mabao matatu.

Gor walipewa cheki ya dola 30,000 (milioni 60) kwa kutwaa taji hilo huku Leopards walikabidhiwa dola 10,000 (milioni 23) kama zawadi ya mshindi wa pili.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *