Kitaifa

Hakimu ataka upelelezi kesi ya Aveva, Kaburu ukamilike haraka

on

Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Victoria Nongwa amewataka mawakili wa Jamhuri kukamilisha haraka upelelezi wa kesi inayowakabili viongozi wa Simba, Evans Aveva na Geoffrey Nyange ‘Kaburu’.

Aveva ambaye ni Rais wa Simba na Makamu wake Kaburu wanakabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za klabu pamoja na utakatishaji pesa dola 300,000 ambazo ni zaidi ya Sh 600 milioni.

Kwa mara ya kwanza Aveva na Kaburu walifikishwa mahakamani hapo Juni 29 na kurejeshwa mahabusu kutokana na kesi hiyo kutokuwa na dhamana ambapo leo Alhamisi walipandishwa tena kizimbani ingawa imeahirishwa hadi Julai 20.

Rais Evans Aveva akiingia mahakamani

Kuahirishwa kwa kesi hiyo ni kutokana na upande wa Jamhuri kutokamilisha upelelezi wa kesi hiyo.

Hakimu Victoria aliiambia Jamhuri kukamilisha haraka upelelezi huo ili watuhumiwa wasiendelee kukaa rumande; “Nawaomba mfanye haraka kukamilisha upelelezi wenu maana hii kesi ni ya tangu mwaka Jana mpaka leo hamjakamilisha upelelezi.

“Naomba kesi ambazo hazina dhamana zifanyike haraka sana, si jambo jema kuwakalisha rumande watuhumiwa wakisubiri upelelezi wa muda mrefu,” alisema Hakimu Victoria.

Katika mahakama hiyo ya Kisutu wadau mbalimbali walifika kusikiliza hatima ya kesi hiyo ambayo haikuchukuwa zaidi ya dakika 15 baada ya mawakili wa Jamhuri kuomba wapangiwe tarehe nyingine.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *