Kitaifa

Hakimu Awapiga Mkwara Mawakili wa Malinzi

on

Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Wilbroad Mashauri ametoa onyo Kali kwa mawakili wanaowatetea watuhumiwa Jamal Malinzi, Celestine Mwesigwa na Nsiende Mwanga kuacha mara moja tabia ya kulalamika kwenye vyombo vya habari kama vile wanaonewa.

Juni 29, watuhumiwa hao ambao ni viongozi wa Shirikisho la soka nchini (Tff), walifikishwa mahakamani na taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa nchini (TAKUKURU) kwa tuhuma za kughushi nyaraka za Shirikisho hilo pamoja na kutakatisha pesa.

Kesi iliahirishwa hadi leo Jumatatu baada ya mawakili upande wa serikali kuomba tarehe nyingine kwa kile walichodai kuwa upelelezi haujakamilika jambo ambalo ndilo lililokuwa likilalamikiwa na mawakili wa watuhumiwa hao kuwa wanawaonea.

Akipitia maelezo ya awali yaliyowasilishwa na pande zote mbili wiki iliyopita, Hakimu Mashauri alikubaliana na upande wa Jamhuri kupanga tarehe nyingine ya kusikiliza mashitaka hayo ili kusubiri upelelezi ukamilike.

Wakili Mwandamizi wa Jamhuri, Nassoro Katuga aliomba msaada kwa Hakimu Mashauri ili kuwaonya mawakili wa watuhumiwa kuacha tabia ya kuzungumza na vyombo vya habari wakati taratibu za kisheria zipo wazi.

“Tunaomba Mahakama itoe onyo kwa mawakili wenzetu upande wa walalamikaji kuacha kuzungumza na vyombo vya habari kwamba wanaonewa na ni kama kuilazimisha Mahakama iamue jinsi ambavyo wanataka wao jambo ambalo linaumiza upande mwingine,” alisema Katuga.

Hakimu Mashauri alisema; “Hata mimi nimeona kwenye vyombo vya habari, hiyo tabia ife na kama mnaona kuna uonevu sheria zipo wazi za kukata rufaa Mahakama kuu, hamzuiwi kuzungumza ila angalieni mnazungumza vitu gani,”.

Baada ya kutamka onyo hilo Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Julai 17 na watuhumiwa wamerudishwa rumande.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Sheila Ally

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *