Habari za kuaminika za michezo na burudani kila wakati.

Hatma ya Nsajigwa, Mwandila Yanga mikononi mwa Zahera

0 1,048

HATIMAYE imefahamika kuwa hatma ya ajira za makocha Shadrack Nsajingwa, Noel Mwandila pamoja maafisa wengine wa benchi la ufundi la Yanga ipo chini ya kocha mkuu Mwinyi Zahera.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwanaspoti ambalo ni maarufu kwa habari za michezo nchini, kocha huyo amesema bado hajaamua kama ataendelea nao au la kwavile anataka kwanza kuona utendaji wao.

Kocha Mwinyi Zahera ataendelea na wasaidizi wake au atawapiga chini?
Related Posts
1 of 32

“Kwasasa siwezi kusema kama nitafanya hivyo au hapana, nataka kuona ubora wa kila msaidizi wangu nitaangalia rekodi zao, lakini pia ufanisi wao katika muda huu nitakaokuwa nao kama nitaona umuhimu wa kufanya hivyo,” alisema.

Taarifa zinadai kuwa uongozi wa Wanajangwani hao ulimweleza Zahera kusudio lao la kufanya mabadiliko katika benchi kabla hata yeye hajawasili lakini aliwaomba wasubiri kwanza.

Kocha huyo raia wa Ufaransa mwenye asili ya DR Congo alijiunga na mabingwa hao wa Ligi Kuu msimu uliopita mwishoni mwa Aprili akichukua nafasi ya George Lwandamina aliyetimkia ZESCO United ya nchini kwao Zambia.
⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽⚽

Get real time updates directly on you device, subscribe now.

Comments
Loading...