Kimataifa

Hatma ya Wenger Arsenal Kujulikana Alhamisi

on

LONDON, Uingereza
KOCHA wa timu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema mustakabili wake utajulikana Alhamisi wiki hii kama ataendelea kuwanoa Washika Bunduki hao au la kufuatia kupata ubingwa wa kombe la FA wikiendi iliyopita.

Mfaransa huyo anakuwa kocha wa kwanza kutwaa taji la FA mara saba baada ya kuwafunga mabingwa wapya wa ligi kuu ya Uingereza timu ya Chelsea mabao 2-1 juzi Jumamosi.

Wenger 67, mkataba wake unamalizika mwezi ujao ambapo kumekuwa na tetesi kuwa ataendelea kusalia klabuni hapo.

“Nimeitunza medali yangu kwakua ulikuwa usiku wa kipekee. Mengine tutaangalia itakavyokuwa.”

Wenger alisema anajua anachotakiwa kufanya na kuongeza kuwa: “Tuendeleeni kushangilia ubingwa huu na msiwe na shaka kuhusu mustakabali.”

 

Kocha huyo aliiambia BBC kuwa: “Tutakuwa na kikao cha kesho Jumanne na keshokutwa Jumatano na siku ya Alhamisi kila kitu kitakuwa wazi.”

Inafahamika kuwa mkutano wa kesho sio rasmi kwa bodi lakini mustakabali wa Wenger utajadiliwa na Wakurugenzi wa klabu hiyo.

Mabao ya Alexis Sanchez na Aaron Ramsey yalitosha kuipa ubingwa Arsenal dhidi ya moja la Diego Costa mchezo uliofanyika kwenye uwanja Wembley.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *