Kitaifa

HENRY JOSEPH: Mimi wa hapa hapa Mtibwa

on

KIUNGO mkongwe wa Mtibwa Sugar ya mkoani Morogoro Henry Joseph ataendelea kuonekana na ‘Wakata miwa’ hao msimu ujao baada ya kukiri kuwa hatoenda popote.

Nahodha huyo wa zamani wa Taifa Stars  alisema hafikirii kuondoka Mtibwa katika kipindi hiki cha usajili ambapo anajipanga kuisaidia kufanya vizuri katika ligi msimu ujao.

Kiungo huyo ameiambia BOIPLUS kuwa akili yake kwa sasa ipo Mtibwa na amekiri kuwa hana sababu ya kutimka klabuni hapo katika siku za karibuni.

“Nipo Mtibwa na nitaendelea kuwa hapa, sifikiri kama naweza kuondoka katika siku za karibuni,” alisema Henry.

Akizungumzia kuhusu kuondoka kwa wachezaji wa kikosi cha kwanza kama Salim Mbonde na Ally Shomari waliojiunga na Simba, kiungo huyo mzoefu alisema haoni kama timu yao itayumba kutokana na uimara wa benchi la ufundi katika kutafuta watakaoziba nafasi zao.

“Sioni kama tutayumba, nadhani hilo ni suala la kocha kuangalia sehemu yenye mapungufu na kurekebisha. Hao walioondoka nafasi zao zitazibwa kwakua wachezaji wapo wengi na wenye uwezo,” alisema Henry.

Mtibwa imekuwa timu inayotoa nyota wengi kwenda timu kongwe ambapo msimu uliopita wachezaji Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin na Mohammed Ibrahim waliondoka na kujiunga na Simba.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *