Kitaifa

Hii Ndio Gari Iliyomfanya Samatta Agome Kucheza Simba

on

UNAKUMBUKA sakata la Mbwana Samatta kugoma kuanza kuitumikia klabu ya Simba akidai kukabidhiwa kwanza gari aliyoahidiwa?, basi leo kamera ya BOIPLUS imelinasa gari hilo ambalo linagonga mzigo hadi leo.

Samatta alisajiliwa na Simba mwezi Juni 2010 lakini hakuanza kuitumikia timu hiyo kufuatia mgomo baridi aliouweka akishinikiza uongozi wa timu kumkabidhi gari waliyoweka kwenye makubaliano ya mkataba wao

Ilipofika Disemba 2010 vigogo wa Wekundu hao walimkabidhi gari dogo aina ya Mitsubish Pajero ndipo nyota huyo ambaye sasa anakipiga na KRC Genk ya Ubelgiji alijiunga na timu akicheza mechi ya kwanza ya kirafiki dhidi AFC Leopards ambapo alitupia bao moja jingine likifungwa na Ally Ahmed Shiboli

Ilipofika Mei 2011 Straika huyo alijiunga na TP Mazembe ya DR Congo. Maisha ya Samatta yalianza kubadilika, pichani kulia ni moja ya magari yake mapya kadhaa ya kutembelea anayomiliki huku Pajero akiwa amemkabidhi kaka yake

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *