The sports Hub

Hivi Hapa Vikosi Viwili Simba, Kuna cha Waarabu na cha Mapinduzi

0 694

SIMBA wamekigawa kikosi chao mara mbili ili kupata kitakachopambana na JS Saoura katika mchezo wa hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika huku wengine wakisalia mjini Zanzibar kusubiri mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi.

Maamuzi hayo yalikuja baada ya ratiba kuingiliana ambapo mchezo dhidi ya Saoura utapigwa Januari 12 jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku moja tu baada ya timu hiyo kucheza mechi ya nusu fainali ya Mapinduzi mjini Zanzibar.

Kama Simba wataingia fainali maana yake ni kwamba watacheza mechi hiyo kisiwani Pemba siku moja tu baada ya kumalizana na Waarabu.

Wachezaji walioelekea Dar es Salaa ni;
1. John Bocco
2. Aishi Manula
3. Shiza Kichuya
4. Meddie Kagere
5. Nicolas Gyan
6. Pascal Wawa
7. Clatous chama
8. Emmanuel Okwi
9. Haruna Niyonzima
10. James Kotei
11. Deogratius Munishi
12. Hassan Dilunga
13. Juuko Murshid
14. Rashid Juma
15. Mohamed Hussein
16. Mzamiru Yassin
17. Said Ndemla.

Wachezaji wa Simba wakiondoka mjini Unguja kuelekea Dar es Salaam

Wachezaji waliobakia kwa ajili ya kuungana na timu ya vijana kucheza Nusu Fainali ya Mapinduzi ni;

1. Adam Salamba
2. Mohamed Ibrahim
3. Ali Salim
4. Zana Coulibaly
5. Asante Kwasi
6. Paul Bukaba
7. Yusuf Mlipili
8. Abdul Seleman.

 

Get real time updates directly on you device, subscribe now.