Kitaifa

Hofu ilivyomuondoa Stars Msuva

on

HOFU ya kukosa kusajiliwa na klabu ya Difaa Hassani El Jadidi (DHJ FC) inayoshiriki ligi kuu nchini Morocco imemfanya winga wa Yanga Simon Msuva ashindwe kusafiri na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars” kwenda nchini Rwanda.

Stars itapambana na timu ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’ katika mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) ambapo katika mchezo wa awali uliopigwa CCM Kirumba jijini Mwanza, timu hizo zilitoka sare ya bao moja.

Msuva anatarajiwa kusaini mkataba na El Jadidi ambapo juzi zilitoka taarifa kuwa dirisha la usajili nchini humo lingefungwa kesho Ijumaa hivyo TFF ikamruhusu Msuva kuondoka kambini ili asafiri kwenda kumalizana na waarabu hao.

Simon Msuva akipiga krosi mbele ya beki wa Amavubi katika mchezo wa awali

Afsa habari wa TFF, Alfred Lucas ameiambia BOIPLUS kuwa walimruhusu Msuva kuondoka ili asipoteze nafasi ya kucheza nje lakini baadae wakaambiwa dirisha hilo litafungwa Agosti 14.

“Ni kweli tulimruhusu mwanzo ingawa baadae tukapata taarifa kuwa dirisha litafungwa Agosti 14, hivyo ataondoka mchana wa leo kwenda kuungana na wenzake Kigali,” alisema Alfred.

Stars itapambana na Amavubi Julai 22 katika uwanja wa Amahoro jijini Kigali mchezo utakaoanza majira ya saa 10 (Rwanda) ambayo ni sawa na saa 9 alasiri kwa hapa nchini.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *