The sports Hub

Huu Hapa Ubabe wa Yanga Afrika Mashariki na Kati

Hakuna cha Al Hilal wala Gor Mahia

0 227

KLABU ya Yanga ya jijini Dar es Salaam imetwaa ubingwa wa Tanzania mara 27 hiyo ikiwa ni mara nyingi zaidi ya timu yoyote kutoka nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati zikiwemo Kenya, Uganda, Tanzania, Sudan, Rwanda na Burundi.

Klabu hiyo iliyoanzishwa Februari 11, 1935 ilipata matokeo mabaya 1936 hali iliyopelekea mgogoro mzito uliozua mpasuko na baadhi wanachama/mashabiki kuunda timu nyingine iliyojulikana kwa jina la Queens ambayo baadae ilibadilishwa jina na kuitwa Sunderland kabla ya jina la sasa la Simba SC.

Yanga ilitwaa ubingwa wa Tanzania Bara kwa mara ya kwanza 1968 na kombe lao la mwisho (la 27) walilitwaa msimu wa 2016/17 wakiendelea kuwa wababe kwa timu zote za ukanda huu. (…inaendelea chini ya matangazo).

Al_Hilal
Kikosi cha Al Hilal ya Sudan

Klabu inayofuatia kwa karibu ni anayochezea mtanzania Thomas Ulimwengu, Al Hilal ya Sudan ambayo ni kongwe zaidi ya Yanga ikianzishwa Februari 13, 1930 yenyewe ikiwa ndio kinara nyumbani kwao baada ya kutwaa mataji 26 ya Ligi Kuu nchini humo.

Katika orodha hiyo ya Wababe wa soka timu inayofuata kwa kutwaa ubingwa mara nyingi nchini kwao ni Vital’O ya Burundi yenye mataji 20 huku nafasi ya nne ikienda kwa wababe wa Kenya, Gor Mahia ambayo licha ya uchanga wake (ikianzishwa Februari 17, 1968), juma lililopita ilifanikiwa kutwaa ubingwa wake wa 17 sawa na APR ambayo haifikiwi na yeyote ndani ya Rwanda.

SC Villa iliyomuibua mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi inashika mkia katika vigogo wa nchi za ukanda huu yenyewe ikiwa imechukua taji la Ligi Kuu mara 16 zaidi ya timu yoyote nchini Uganda.

Get real time updates directly on you device, subscribe now.