Kitaifa

Huyu hapa mwamuzi Everton, Gor Mahia

on

MWAMUZI Israel Nkongo ndiye aliyepewa dhamana ya kuamua mchezo wa kihistoria wa kirafiki kati ya Everton ya Uingereza dhidi Gor Mahia kutoka Kenya utakaofanyika keshokutwa Alhimisi kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Nkongo ambaye ana beji ya Shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA), atasaidiwa na Ferdinand Chacha, Frank Komba wakati mwamuzi wa mezani akiwa Heri Sasii na Kamishna wa mchezo ni Michael Wambura.

Mkurugenzi wa Kampuni ya SportPesa nchini ambao ndio waratibu wa mchezo huo Abass Tarimba amewaambia Waandishi wa Habari kuwa maandalizi ya mechi yamekamilika na kinachosubiriwa ni timu hizo kuwasili kwa mtanange huo.

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika, usalama umeimarishwa kutokana na ukubwa wa mchezo wenyewe hivyo niwaombe mashabiki kujitokeza kwa wingi,” alisema Tarimba.

Kwa upande wake Meneja Miradi wa Kampuni ya Selcom ambao ndio wanaotoa tiketi za mchezo huo Gallus Runyeta amesema tayari zoezi la uuzaji tiketi linaendelea na kwa mtu asiye na kadi anaweza kuwahi mapema siku ya mchezo zitapatikana uwanjani.

Nae Afisa Usalama wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), Inspekta Hashim Abdallah amewataka mashabiki watakaojitokeza kwenye mchezo huo kuachana na mahaba kwa wachezaji ikiwemo kwenda kuwakumbatia kwakua hawataruhusiwa kufanya hivyo.

“Mshambuliaji Wayne Rooney atakuwepo kwenye msafara huo, kuna watu watataka kwenda kumkubatia jambo ambalo halitaruhusiwa,” alisema Inspekta Hashim.

Gor watawasili nchini leo saa nane mchana huku Everton wakiingia kesho saa tatu asubuhi.

Viingilio katika mchezo huo ni shilingi 8000 kwa VIP B na C huku mzunguko ukiwa 3000 ambapo VIP A kiingilio chake bado hakijatajwa.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *