Kitaifa

JAMHURI DODOMA: Nje ‘Ntiti’, Ndani ‘Ntiti’

on

Hii ndio fainali bwana…..saa sita tu nje kumejaa, ndani hakuna nafasi. Idadi ya mashabiki waliojitokeza kuhudhuria mchezo wa fainali kati ya Simba na Mbao FC imekuwa kubwa kuzidi ilivyotarajiwa huku kukiwa na tetesi kuwa muda wowote mageti ya uwanja huo yatafungwa.

Hali ilivyokuwa ndani ya uwanja majira ya saa 6 mchana

BOIPLUS ambayo imepiga kambi uwanjani hapa kwa ajili ya kuripoti kila kinachoendelea kabla na baada ya mchezo wenyewe imeshuhudia mamia ya mashabiki hao wakiingia wakiwa na jezi za timu zao pamoja na mavuvuzela .

Usalama umeimarishwa kwa kiasi kikubwa huku ikishuhudiwa askari wengi kutoka jeshi la Polisi wakifanya kazi yao kuhakikisha amani na utulivu inatawala.

Nje ya uwanja watu ni wengi kuliko waliopo ndani

Imedaiwa kuwa endapo mashabiki watakuwa wamejaa kabla ya mechi kuanza basi mageti yote yatalazimika kufungwa na kutoruhusu shabiki yoyote kuingia kuangalia mechi hiyo.

Tayari mpaka sasa eneo linalokaliwa na mashabiki wanaoingia kwa viingilio vya bei ya chini yamejaa huku likiwa limebaki eneo la jukwaa kuu pekee ambako viingilio ni Sh 15000 na 20000.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Boiplus Media

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *