Kimataifa

JEURI YA SPORTPESA: Everton Yaongoza Kumwaga ‘Mkwanja’ Uingereza

on

KAMA ulidhani mamilioni ya kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Sportpesa yamewapa kiburi Simba, Yanga na Singida United tu basi umejidanganya, Everton imeonyesha inajua ‘kuyatumbua’ vizuri zaidi.

Ni kama mshangao kuona hadi sasa Everton inayodhaminiwa na Sportpesa ndio timu inayoongoza kwa kutumia pesa nyingi zaidi kwenye usajili baina ya timu za ligi kuu nchini Uingereza katika dirisha hili la majira ya joto.

Jeshi hilo la Ronaldo Koeman lilimaliza katika nafasi ya sita msimu uliopita na sasa wameonyesha nia ya dhati ya kuingia katika timu nne bora msimu huu ili wafanikiwe kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Gor Mahia wakishangilia ubingwa wa Sportpesa Super Cup uliowapatia nafasi ya kucheza na Everton

Hadi sasa Everton wametumia kiasi cha paundi 83 milioni ambacho ni zaidi ya sh 230 bilioni pesa ambayo haijawahi kutumika majira ya joto klabuni hapo.

Tetesi za kuuzwa kwa Romelu Lukaku kwenda Manchester United kwa kiasi cha paundi 75 milioni zinaashiria kuwa timu hiyo itaendelea kutumia pesa zaidi katika usajili hasa kwenye kupata straika wa kuziba pengo la mbelgiji huyo.

Everton inatarajiwa kutua nchini wiki ijayo ikiwa na kikosi chake kizima kupambana na Gor Mahia ya Kenya Julai 13 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salam.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *