Kimataifa

Jezi Mpya Chelsea Zavuja Kabla ya Kutangazwa Rasmi

on

SIKU moja kabla mabingwa wa Uingereza, Chelsea hawajafungua milango ya duka lao kutangaza jezi mpya za msimu ujao, picha za jezi ya kipa na za mazoezi zimeonekana mitandaoni.

Mtandao wa FootyHeadlines.com umetoa picha ya jezi ya kipa huku @FK_Sport wakitoa picha ya jezi zitakazotumiwa na wachezaji wa timu hiyo mazoezini ambazo zinaonekana bado zitakuwa na nembo ya mdhamini ambaye ni kinywaji cha kuongeza nguvu cha Carabao.

Mashabiki wa Chelsea watalazimika kusubiri hadi asubuhi ya Julai mosi kujua kama jezi zilizovunja ndizo zenyewe au zitakuwa tofauti.

USISAHAU KU LIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI
Washirikishe rafiki zako habari hii kwa kuwatumia kupitia mitandao ya kijamii hapa chini

About Karim Boimanda

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *